Recent Posts

KWA MATANGAZO WASILANA NA UONGOZI WA Deopa TV NO:0765-743393 AU 0658508231, EMAIL:deostivu123@gmail.

Jux na Vanessa Mdee watangaza balaa lingine kwa mashabiki wao wa DR Congo, Rwanda na Burundi

Wakati mashabiki wa Vanessa Mdee na Jux nchini Tanzania wakiendelea kukata kiu ya burudani kupitia tamasha la wawili hao linalokwenda kwa jina la ‘In Love and Money Tour’, tayari wawili hao wametangaza habari njema kwa mashabiki wao wanaoishi nje ya nchi.
Habari yenyewe ni kwamba wawili hao wameahidi kufanya ziara yao hiyo ya muziki nchini DR Congo, Rwanda na Burundi hii ni baada ya kumaliza show yao ya mwisho Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Wasafi Tv, Jux amesema kuwa “Hii show inaendelea tukitoka Dar tunaenda Rwanda, tukitoka Rwanda tunakwenda Burundi na tukitoka Burundi tunakwenda Congo.
Jux amefunguka hayo jana mkoani Arusha muda mfupi baada ya kutumbuiza kwenye ziara yao ya muziki ya ‘In Love and Money Tour’  jijini humo.

Hii ndio show kali zaidi ya Diamond Platnumz kuwahi kutokea, awaimbisha kiswahili Wafaransa kisiwani Mayotte

Kwa sasa ukitaja majina ya wasanii 10 bora wanaofanya vizuri barani Afrika huwezi kuacha kumtaja Diamond Platnumz hii ni kutokana na kuongezeka kwa wigo mpana wa mashabiki wake.

Hili la kuongezeka kwa idadai ya mashabiki linajidhihirisha hata pale Diamond anapokuwa nje ya Tanzania hususani katika mataifa ambayo hayaongei Kiswahili.
Jana Julai 28, 2018 Diamond Platnumz alikuwa katika visiwa vya Mayotte nchini Ufaransa ambapo aliweza kutumbuiza nyimbo zake zote tena zile ambazo hajafanya kolabo na jambo la kufurahisha licha ya asilimia 99% ya wananchi wa Mayotte kuzungumza Kifaransa lakini waliweza kuimba naye nyimbo zote kwa kiswahili.