Recent Posts

KWA MATANGAZO WASILANA NA UONGOZI WA Deopa TV NO:0765-743393 AU 0658508231, EMAIL:deostivu123@gmail.

Mbappe husaidia Ufaransa kuwapiga Argentina 4-3


Kylian Mbappe alifunga mabao mawili ndani ya dakika nne na kumtuma Ufaransa kwenye Kombe robo fainali kwa kushinda 4-3 dhidi ya Argentina siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alifunga mabao ya tatu ya Ufaransa kwa dakika ya 64 na kufungwa kwa dakika nne baadaye na kumaliza baridi ili kuanzisha mgongano wa robo ya mwisho na Uruguay au Portugal, ambao watakutana baadaye Jumamosi.
Benjamin Pavard pia alitoa mechi nzuri kwa Ufaransa baada ya adhabu ya dakika ya 13 ya Antoine Griezmann kufungua bao.
Malengo ya Argentina yalikuja kutoka kwa Angel Di Maria, ambaye alifanya mshangao mzuri wa muda mrefu mechi ya dakika ya 41 ili kuwapiga kiwango cha 1-1, kabla ya Gabriel Mercado kuwaweka mbele baada ya mapumziko. Sergio Aguero anayeiweka nafasi ya tatu aliongeza muda wa tatu wakati wa kuacha.

Avril apost picha ya mtoto wake kwa mara ya kwanza



Staa maarufu kutokea  Nairobi, Kenya Avril ameonyesha picha akiwa na mwanae kwa mara ya kwanza katika ukurasa wake wa instagram ikiwa hakuwahi kufunguka kuhusiana na ujauzito wake wala mzazi mwenzake.
Staa huyo aliweka siri kuhusiana una ujauzito wake na hakutaka ishu hiyo kuwa kwenye mitandao ya kijamii na kuongelewa na watu na hivyo baada ya kupata mtoto wake wa kwanza miezi kadhaa iliyopita aliamua kuweka picha hiyo ili kushare good news na mashabiki zake.
Kupitia ukurasa wake wa istagram Avril aliandika “Yote yana thamani yake” akiwa kambeba mtoto wake.

Pete Davidson baada ya kumvalisha pete Ariana Grande asema hiviii


Mpenzi wa sasa wa staa wa muziki nchini Marekani Ariana Grande amekubali ishu ya kumvalisha pete ya uchumba mwanadada huyo katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha television ambacho ni maarufu nchini Marekani  The Tonight Show.
Pete Davidson ambaye ni mchumba wa sasa wa staa huyo ameongelea furaha aliyonayo ikiwa ni miezi mitatu tu tokea wajuane na Ariana Grande na kumvalisha pete ya uchumba na kusema kuwa ni kitu ambacho hakukitegemea katika maisha yake na anahisi kama ameibuka mshindi katika mashindano.
Pete Davidson alisema kuwa “Ni kitu kizuri sana kwa sababu ukipita mtaani vijana wengi wanakupa heshima kwa kitendo hicho”

Paul Okoye afunguka maisha mapya bila Pacha wake


Superstar Paul Okoye maarufu kama Mr. P kutokea Nigeria amefunguka kupitia mahojiano aliyofanya na The Koffee Gang show kwenye Hot 93.3 FM nchini humo na kuzungumzia kuhusu maisha yake mapya kama solo artist baada ya kuachana na kundi la Psquare.

Paul Okoye amekielezea chombo hicho kuwa hakuogopa kuanza upya kwenye maisha ya muziki alijua kuwa kuna maisha mapya mbeleni pia alisema kuwa hapendi kujisifia kuhusiana na muziki anaoufanya kwa sababu ana vipaji vingi ikiwa ana uwezo wa kuproduce muziki mwenyewe.

“Niliacha kundi la Psquare likiwa na wafuasi karibia milioni moja kwenye mtandao wa youtube na sikuogopa kuanza upya nilijua kuna kitu kizuri mbeleni , lakini nimesonga mbele na nimependa,  pia napenda nguvu niliyoiweka” 

Tip Top Connection hatuko bize kama WCB – Dogo Janja

Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amefunguka mchango wa Babu Tale ndani ya Tip Top Connection kwa sasa.
Hii ni baada ya Babu Tale kuwa sehemu ya menejimenti ndani ya lebo ya WCB na kuibua madai kuwa meneja huyo kaitelekeza Tip Top Connection.

Dogo Janja akiwa katika la Tamasha la Kuibua Vipaji vya Muziki mkoani Arusha amesema kuwa hilo halina ukweli wowote kwani wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi.
“Hapana sio kweli, Babu Tale anasimamia kazi zangu sana sana ila kwamba huku Tip Top sisi hatuko bize kama Wasafi ndio maana unaoa muda wote yupo kule, hatuna matukio,” amesema.
“Lakini nikiachia wimbo utaona redioni nitaenda na Babu Tale, so mimi sina matukio mengi ndio maana kwenye kazi zangu anakuwa mara chache sana pale ninapomuhitaji,” ameeleza Dogo Janja.
Hata hivyo licha ya Dogo Janja kuwa Tip Top Connection anapata mchango mkubwa kutoka kwa Manzese Music Baby (MMB), menejimenti ambayo imeanzishwa na Madee

Diamond anusurika katika ajali nchini Marekani

Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amenusurika katika ajali ya gari nchini Marekani ambapo upo kwa ajili ya tour ya albamu yake ‘A Boy From Tandale’
Muimbaji huyo amepata ajali hiyo wakati akitokea kwenye show. Kupitia mtandao wa Instagram ameandika;


Dah Tumepata ajali na kunusurika kufa usiku wa leo wakati tunatoka kwenye show….ila Mwenyez Mungu ametupa nafasi nyingine tena ya kuishi na kuendelea kushikana mkono na vijana wenzangu mtaani kwa pamoja tuziokoe familia zetu duni🙏🏻….
Video Player
00:00
00:21

Diamond ni ndiye mwanzilishi na mmiliki wa label ya WCB ambayo inasimamia wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava na Mbosso.

Banana Zoro aupamba usiku wa tuzo

Muimbaji wa muziki, Banana Zoro ameupamba usiku wa tuzo za ligi kuu zilizofanyika ukumbi wa Mlinacty kwakufanyika vibao kadhaa kikiwemo cha Mama.




Mchezaji bora wa VPL 2018, John Bocco atangaza vita msimu ujao

Mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18, John Bocco amewashukuru wachezaji wenzake kwa mchango wao katika kumuwezesha kutwaa tuzo hiyo na kuahidi kufanya vema zaidi msimu ujao

Avril ametuonyesha picha ya mtoto wake kwa mara ya kwanza

Staa maarufu kutokea +254 Nairobi, Kenya Avril ameonyesha picha akiwa na mwanae kwa mara ya kwanza katika ukurasa wake wa instagram ikiwa hakuwahi kufunguka kuhusiana na ujauzito wake wala mzazi mwenzake.

Staa huyo aliweka siri kuhusiana una ujauzito wake na hakutaka ishu hiyo kuwa kwenye mitandao ya kijamii na kuongelewa na watu na hivyo baada ya kupata mtoto wake wa kwanza miezi kadhaa iliyopita aliamua kuweka picha hiyo ili kushare good news na mashabiki zake.
Kupitia ukurasa wake wa istagram Avril aliandika “Yote yana thamani yake” akiwa kambeba mtoto wake.

Habari kubwa za Magazeti ya TZ leo June 22, 2018 Udaku, Michezo na Hardnews

Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania June 22, 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa  kwenye magazeti
















NIGERIA 2-0 Iceland



    Timu  ya Taifa ya Nigeria imeibuka na ushindi wa magoli mawili dhidi ya Iceland.
    Magoli yote yamefungwa na Ahmed Musa katika kipindi cha pili na kuifanya nigeria kusonga mbele katika michuano ya kombe la dunia inayo endelea nchini Russia.

    Mzee Majuto arejea nchini akitokea India

    Msanii wa filamu Bongo, Mzee Majuto amerejea nchini akitokea katika matibabu nchini India.

    Mara baada ya kutoa nchini Mzee Majuto amesema hali yake ya kiafya imetengamaa ukilinganisha na hapo awali. Hii ni kutokana na huduma alizopatiwa ambazo ameeleza ni za kisasa zaidi ukilinganisha na za hapa nchini.
    Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa anahitaji kupumzika zaidi na hana mpango wa kurejea katika sanaa ya maigizo.
    Mzee Majuto aliondoka nchini May 4, 2018c kuelekea India. April 28, 2018 alirudishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo awali alikuwa akipatiwa matibabu kabla ya kuhamishiwa hopitali ya binafsi, Tumaini, ndipo akapelekwa India

    Argentina yachapwa 3-0, mashabiki wa Lionel Messi wakosa amani!



    Kipigo cha Argentina cha goli 3-0 dhidi ya Croatia kimewachanganya kabisa mashabiki wa mshambuliaji wa timu hiyo na klabu ya Barcelona, Lionel Messi huku mmoja kati ya mashabiki hao wakimshauri mchezaji huo kubadili uraia.


    Rapper Jimmy Wopo afariki kwa kupigwa risasi


    Baada ya taarifa za Rapper chipukizi Xxxtentacion kufariki dunia kwa kupigwa risasiJune 18,2018 hii ni taarifa nyingine ya msiba kutoka kwa Rapper Jimmy Wopo ambaye amefariki muda mchache baada ya kupigwa risasi June 18,2018.
    Jimmy Wopo amepigwa risasi na kufariki na watu wasiojulikana akiwa kwenye mji wa Piitsburgh na imeripotiwa  kuwa katika tukio hilo kuna baadhi ya watu wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali na hali zao kwa sasa zinaendelea vizuri.
    Rapper huyo enzi za uhai wake ametambulika na ngoma zake kibao zikiwemo Elm Street, Prime Time, Lost, Ayo na nyingine nyingi na amefariki akiwa na umri wa miaka 21.

    Alichoandika Vanessa juu ya tour INLOVE & MONEY Mwanza



    Wakali kutokea kwenye Bongo Fleva Vanessa Mdee pamoja na Juma Jux ambao pia ni wapenzi wanakuja na tour yao ya Inlove & Money ikiwa inahusisha album ya Juma Jux i nayoitwa Inlove na album ya Vanessa Mdee ambayo ndio Money Mondays (Inlove &Money).

    Tour hii itahusisha mikoa mbalimbali na pia wasanii ambao wapo chini ya record label ya Mdee Music watapewa nafasi ya kuperform katika mikoa hiyo, mkoa wa kwanza kuhusishwa ni Rock City Mwanza ambapo Vanessa Mdee pamoja Juma Jux watawasili na kutoa burudani June 30,2018.
    Mkoa wa Mwanza ndio utafungua tour hiyo ya Inlove & Money ikiwa ndio itakua mara ya pili kwa Vanessa Mdee pamoja Juma Jux kufanya performance katika mkoa huo ambapo mara ya kwanza ilikuwa kwenye Fiesta 2017.
    Instagarm post ya vanessa ilikuwa hiviii

    Vanessa amjibu shabiki wake aliyemuambia hawezi kuimba na live band........


    Staa wa Bongo Fleva Vanessa Mdee ameamua kumjibu shabiki ambaye amemkosoa katika kucomment na kudai kuwa Vanessa Mdee hajui kuimba na live band, hivyo ni sawa na kupoteza muda wake pamoja na hela kwenda kutazama live show yake.
    Comment ya shabiki huyo imejibiwa na Vanessa Mdee baada ya kutangaza kuhusiana na tour yake ya Inlove & Money katika mkoa wa Mwanza na kusema kuwa Ndio maana umepoteza muda wako kwa msanii ambae anapoteza posts na live shows ambaye unamfatilia, Mungu akubariki mpendwa”
    Basi mambo yalikuwa iviiiii

    Basata watangaza kuufungia wimbo mpya wa Sugu

    Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limetangaza rasmi kuufungia wimbo mpya ‘#219’ wa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu
    .
    Basata wametangaza hilo kupitia barua yao waliyoitoa Jumanne hii ambayo inaelezea sababu za kuufungia wimbo huo ni kutokana na kuwa na maneno ya uchochezi na kuhatarisha amani pamoja na utengano katika jamii.
    Mbali na kuufungia wimbo huo, Basata wamemuonya msanii huyo kwa kumtaka kuacha mara moja kuutangaza na kuisambaza ngoma hiyo. Soma barua hiyo hapo chini

    Senegal warudisha matumaini ya Waafrika kwenye michuano ya Kombe la Dunia

    Timu ya taifa ya Senegal leo imerudisha matumaini ya Waafrika kunako michuano ya kombe la Dunia kwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Poland .
    Goli la kwanza la Senegal limepatikana kwa beki wa Poland, Thiago Cionek kujifunga kunako dakika ya 37 huku goli la pili la likitupiwa na Mbaye Niang.
    Goli pekee la kufutia machozi la Poland inayoongozwa na Lewandowski likifungwa na Grzegorz Krychowiak kunako dakika ya 86 ya mchezo.
    Senegal inakuwa timu ya kwanza kutoka bara la Afrika kupata ushindi kwenye michuano ya kombe la dunia ya mwaka huu nchini Urusi.
    Je, Senegal ya mwaka huu inaweza kuvunja rekodi yao ya mwaka 2002 ya kufika robo fainali ya michuano hiyo ya Kombe la dunia?

    Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema kuwa amevutiwa na kiwango kilichoonyesha na kikosi chake dhidi ya Tunisi

    Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema kuwa amevutiwa na kiwango kilichoonyesha na kikosi chake dhidi ya Tunisia hatakama vijana hao wa ‘Three Lions’ wangelazimishwa sare ya 1 – 1 kabla ya Harry Kane kutupia la pili na laushindi.
    Katika dakika za nyongeza kabla mchezo huo kumalizika, Kane aliipatia Uingereza bao la pili na la ushindi na kufanya matokeo kuwa 2 – 1 kwenye mechi hiyo ya kundi G kwenye dimba la Volgograd.
    Southgate amesema kuwa kwa upande wake amevutiwa na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na vijana wake kwakuwa wametengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza.
    “Hatakama mchezo ungekuwa sare ya 1 – 1 bila shaka ningejivunia na kiwango kilichoonyeshwa. Nilizungumza nao sana kuongoza kwenye mechi hii na kiwango bora ndiyo jambo muhimu zaidi nililowasisitizia kwakuwa hicho ndicho kitu ambacho unaweza kuhakikisha unakuwa nacho ndani ya kikosi.” amesema Southgate.

    “Tuliongoza ndani ya uwanja jambo ambalo liliashiria kuwa walizingatia ujumbe wangu. Tulizungumza asubuhi kuwa ndani ya mchezo.” Nilazima tuufurahie usiku wa leo lakini bila kujisahau sana kwakuwa siku nne,tano zijazo tutakuwa na mchezo dhidi ya Panama hivyo nilazima tufanye maandalizi ili kuweza kupata matokeo.