Recent Posts

KWA MATANGAZO WASILANA NA UONGOZI WA Deopa TV NO:0765-743393 AU 0658508231, EMAIL:deostivu123@gmail.

Mimi simkubali mwanamuziki yeyote – Mr. Nice

Msanii wa muziki Bongo, Mr. Nice amedai kuwa hamkubali msanii yeyote zaidi yake hata akipewa fursa ya kutaja orodha ya wasanii watano anaowakubali nafasi hizo zote atajipatia yeye.

Muimbaji huyo aliyetamba na style ya Takeu amesema hayo nchini Rwanda alipokuwa akifanya show weekend iliyomalizika. Mr Nice amewataja wasanii anaowakubali ni Lady Jaydee, Professor Jay na Jose Chameleone kutoka nchini Uganda.
“Lady Jaydee ni legendari mwenzangu, ni wanamuziki mwenzangu, hivyo hivyo kwa Professor Jay,” amesema.
“Jose Chameleone is Friend of mine ambaye ninaweza nikavua viatu vyangu nikamwambia vaa Jose, dah huyu mtu unajua mimi simkubali mwanamuziki yeyote, namkubali Mr. Nice tu ukiniambia nikupe top five yangu msanii wangu nitakuambia ni Mr. Nice,” amesisitiza.
Mr. Nice kwa sasa anafanya vizuri na ngoma inayokwenda kwa jina la Tuheshimian

Harmonize ft Diamond platnumz - KwaNgwaru

DIAMOND PLATINUM AKIIMBA WIMBO WAO MPYA NA Harmonize

Harmonize ft Diamond platnumz - Kwa Ngwaru (OFFICIAL VIDEO

TAZAMA WIMBO Harmonize ft Diamond platnumz - Kwa Ngwaru

MAGAZETI YA LEO 29/3/2018





















MAGAZETI YA LEO TARE 28/3/2018





















Viongozi wa Chadema akiwemo Mh. Mbowe wawekwa mahabusu

“Viongozi Wakuu wa Chadema akiwepo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao wamewekwa mahabusu.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA, Tumaini Makene imeeleza kuwa Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo ila Mawakili wanashughulikia.
Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi,” amesema Makene.
Viongozi walioripoti Polisi ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Freeman Mbowe,Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vicent Mashinji ,Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika,salum Mwalimu na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake (Bawacha)Esther Matiko.

MAGAZETI YA LEO TARE 27/3/2018