Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amepata majeraha ya kifundo cha
mguu wa kulia (Ankle) wakati akiwa kwenye mazoezima timu hiyo hapo
jana.
Daktari wa kikosi hicho cha Simba, Yassin Gembe amesema kuwa Mkude
ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia na haonekani kuwa amepata
majeraha makubwa.
“Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kwa vipimo vya awali
sio majeraha makubwa sana, ila kesho ndio tutatoa taarifa kamili
kuhusianana na hali yake kwa ujumla ila kwa sasa napenda kusema
anaendelea vizuri kutoka katika matibabu ya awali tuliyompatia” amesema
Gembe.
Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa kiungo huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku mbili hadi tatu.
No comments:
Post a Comment