Muigizaji huyo amemshukurua RC Makonda kwa kumtia moyo kwani ni kitu ambacho anakihitaji sana kwa kipindi hiki.
“Lakini pia naomba nikuahidi, sitokuangusha maana kumuangusha RC wako nako sio pambe kabisa,” amesema Wema.
“Picha ya hapo juu uliyoomba ni mmiliki halali wa Filamu ya Heaven Sent ambaye kajisajili Cosota na Bodi ya Filamu, anazo haki miliki zake zote na ndio aliyeshinda Best Actress 2018 kwa kuwa amekidhi sababu zote za kuwa Mshindi,” amesema.
Wema ameendelea kwa kusema anataka tasnia ya Filamu iwe na watu wenye kujielewa na wenye upeo mkubwa, sio wenye kukurupuka na kuvamia jambo bila kudadavua na kujua ni kitu gani kinatakiwa kufanyika.
“Yote yanawezekana, wasanii ni watu wenye wadhifa mkubwa sana, najivunia kuwa mmoja kati yao. Ninajua hata wewe unajivunia kuwa kati yetu sisi ukiwa kama Mlezi ukituongoza kila leo kutaka tufike sehemu nzuri na Inshallah tutafika,” ameeleza Wema
No comments:
Post a Comment