Recent Posts

KWA MATANGAZO WASILANA NA UONGOZI WA Deopa TV NO:0765-743393 AU 0658508231, EMAIL:deostivu123@gmail.

MTIBWA YAPELEKA UCHUNGU NAMFUA NA KUTUMA SALAAM KWA SIMBA, LIPULI NA MBAO HAKUNA MBABE




Mechi mbili za Ligi Kuu Bara zimepigwa jioni ya leo ambapo katika Uwanja wa Namfua, Singida United ilikuwa ikiikaribisha Mtibwa Sugar FC kutoka Morogoro, huku Mbao FC ikiialika Lipuli FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika mchezo uliopigwa mjini Singida, Mtibwa Sugar imeiadhibu vikali Singida United kwa jumla ya mabao 3-0.

Wafungaji wa mabao hayo ni Kelvin Sabato 22', Salum Kawimbwi 53' na Hassan Dilunga 71'.

Kipingo hicho kinakuwa kuwa ni salaam kwa Simba ambapo Mtibwa watakuwa wanacheza nayo Jumatatu ya Aprili 9 2018 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mtibwa wataanza safari yao kurejea Morogoro kesho tayari kuwakabili Simba siku ya tarehe Aprili 9 2018.

Mbali na mechi hiyo, Mbao FC waliokuwa wenyeji pia jijini Mwanza wamelazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa.

No comments:

Post a Comment