Rais wa Simba SC, Aveva ambaye anasumbuliwa na maradhi kwa muda
mrefu amefika katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi
yake inayomkabili ambapo jana alipaswa kusomewa maelezo ya awali na
mwenzake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Licha ya kusomewa maelezo hayo, kesi hiyo imeahirishwa tena mpaka
Aprili 12 mwaka 2018 kufuatia Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai, kuomba
hati ya mashtaka ifanyiwe mabadiliko.
Swai ameiomba Mahakama kubadilisha hati ya mashtaka kwa kumuongeza
mshtakiwa mwingine ambapo Aprili 12 mwaka 2018 watasomewa maelezo hayo
ya awali.
Taarifa zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikia hapo baada ya upelelezi kukamilika upande wa mashtaka.
Mhusika mwingine anayekabiliwa na kesi hiyo ni Makamu wa Rais wa
Simba, Godfrey Nyange Kaburu ambaye alitinga pia mahakamani hapo leo.
Washtakiwa wote wawili wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi
nyaraka za uongo na utakatishaji wa fedha, kiasi cha USD 300,000.
No comments:
Post a Comment