Recent Posts

KWA MATANGAZO WASILANA NA UONGOZI WA Deopa TV NO:0765-743393 AU 0658508231, EMAIL:deostivu123@gmail.

Rais wa zamani wa Brazil atupwa jela miaka 12, baada ya kupatikana na kosa hili

Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva amehukumiwa kwenda jela miaka 12 na Mahakama ya rufaa nchini humo baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi.
Tokeo la picha la Luiz Inacio Lula da Silva
Luiz Inacio Lula da Silva
Kesi hiyo iliyoongozwa na Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama hiyo ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakiunga mkono.
Kesi hiyo iliyochukua muda mrefu wa uchunguzi baada ya sakata la rushwa lililojulikana kama ‘Operation Car Wash’, hukumu yake imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Kwenye hukumu hiyo, mahakama imebaini kuwa Lula alichukua rushwa yenye thamani Euro 790,000 sawa na bilioni 2.1 .
Lula da silva ni moja ya marais wastaafu waliyoiongoza Brazil ambao bado wanaushawishi mkubwa kwenye siasa za Brazil na amekuwa akitarajiwa kusimama tena kugombea urais wa nchi hiyo kama mgombea huru kwenye uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment