Recent Posts

KWA MATANGAZO WASILANA NA UONGOZI WA Deopa TV NO:0765-743393 AU 0658508231, EMAIL:deostivu123@gmail.

Jux na Vanessa Mdee watangaza balaa lingine kwa mashabiki wao wa DR Congo, Rwanda na Burundi

Wakati mashabiki wa Vanessa Mdee na Jux nchini Tanzania wakiendelea kukata kiu ya burudani kupitia tamasha la wawili hao linalokwenda kwa jina la ‘In Love and Money Tour’, tayari wawili hao wametangaza habari njema kwa mashabiki wao wanaoishi nje ya nchi.
Habari yenyewe ni kwamba wawili hao wameahidi kufanya ziara yao hiyo ya muziki nchini DR Congo, Rwanda na Burundi hii ni baada ya kumaliza show yao ya mwisho Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Wasafi Tv, Jux amesema kuwa “Hii show inaendelea tukitoka Dar tunaenda Rwanda, tukitoka Rwanda tunakwenda Burundi na tukitoka Burundi tunakwenda Congo.
Jux amefunguka hayo jana mkoani Arusha muda mfupi baada ya kutumbuiza kwenye ziara yao ya muziki ya ‘In Love and Money Tour’  jijini humo.

No comments:

Post a Comment